Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, Mfuko wa Taifa wa Utajiri wa Norway umeishauri wizara ya fedha ya nchi hiyo kusitisha uwekezaji katika baadhi ya makampuni, yanayousaidia utawala wa Israel katika kukiuka haki za Wapalestina na kuendeleza ukaliaji wa mabavu wa ardhi zao. Mfuko wa Taifa wa Utajiri wa Norway unapanga kuweka vigezo vigumu zaidi vya maadili ili kusitisha ushirikiano na baadhi ya makampuni ambayo yanausaidia utawala ghasibu wa Israel katika vita vya Ghaza, na kuondoa hisa zake katika makampuni hayo.Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Mfuko wa Utajiri wa Norway ambao kutokana na kuwa na akiba ya dola trilioni 1.7 ndio mfuko mkubwa zaidi wa uwekezaji duniani, unapanga pia kupitia upya hisa zake katika makampuni yanayofanya kazi katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.
342/